RAIS John Magufuli jana, aliungana na maaskofu, mapadre, watawa na waumini wa Kanisa Katoliki kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Mhashamu Askofu Evaristo Chengula, aliyefariki dunia Novemba 21, mwaka huu, huku akimsifu kwa tabia yake ya kusema ukweli kwa kukemea ushoga.
Askofu Chengula alifariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Misa Takatifu ya kumuaga marehemu Askofu Chengula iliyoongozwa na Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, J

Loading...
de Thadaeus Ruwa’ichi, katika Kanisa la Mtakatifu Imakulata lililopo Makao Makuu ya Baraza la Maaskofu, Kurasini jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na mkewe, Anna Mkapa.
Akizungumza baada ya misa hiyo Rais Magufuli alitoa salamu za pole kwa maaskofu wote wa Kanisa Katoliki, mapadre, watawa, waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya na Wakatoliki wote nchini kwa kuondokewa na kiongozi aliyekuwa akifanya vyema kazi yake ya kutangaza injili.
Rais Magufuli alisema pamoja na majukumu yake ya kutoa huduma za kiroho, marehemu Askofu Chengula alisimamia ukweli ikiwamo kupinga hadharani ndoa na mapenzi ya jinsia moja licha ya kuwapo mashinikizo mbalimbali.
Na Mary Mkeu.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MAGUFULI AMSIFU ASKOFU CHUNGULA KUPINGA USHOGA
Reviewed by By News Reporter
on
11/27/2018 07:15:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: