Loading...

WAZIRI UMMY ASEMA AMEJIPANGA VYEMA 2019/20, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini imepitisha vipaumbelea vinane vitakavyofanyiwa kazi katika sekta ya afya kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Hayo yalibainishwa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Ummy Mwalimu,  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kikao cha mwaka cha wadau wa sekta ya afya kujadili vipaumbele vya utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. Vipaumbele vilivyoainishwa na waziri ni:-

- Kuimarisha huduma za afya ya uzazi ya mama na mtoto, lengo likiwa ni kupunguza vifo vya wajawazito
Loading...
rif;">
- Afya za wasichana balehe pamoja na wavulana, kwa kuwa hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya wasichana 10,027 wanapata ujauzito kabla ya kutimiza miaka 18

- Kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

- Kuajiri watumishi katika sekta ya afya pamoja na kuimarisha huduma za afya. Kuhakisha kuwa tunaimarisha upatikanaji wa dawa ikiwa ni pamoja na kufika kwa wakati na kutumika kwa usahihi na dawa muhimu kupatikana katika vituo vya afya kwa asilimia 90.

Na Neema Joshua.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAZIRI UMMY ASEMA AMEJIPANGA VYEMA 2019/20, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE WAZIRI UMMY ASEMA AMEJIPANGA VYEMA 2019/20, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE Reviewed by By News Reporter on 11/27/2018 07:07:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.