Loading...

AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE WAPO HOI GEREZANI

Msanii Amber Rutty  na mpenzi wake ambae wanasota gerezani mpaka sasa kwa kukosa dhamana baada ya kuingizwa selo wakiwa na kosa la kuvujisha video walizojirekodi kinyume na kanuni na hata kuizifanya zikasambaa katika mitandao ya kijamii.

kwa chanzo kinachotoa habari za wawili hao zinasema kuwa wawili hao kwa sasa wameanza kuonekana kudhoofika sana huku sababu kubwa ikihisiwa kuwa wawili hao walikuwa na ugonjwa  wa kifua kikuu.

Moja ya ndugu wa karibu wa Amber Rutty anasema kuwa wawili hao walikuwa wakiumwa ugonjwa huo kabla ya matatzio haya kuwakuta na waliwahi kuzidiwa sana hata kusafirishwa kutoa jijini mpaka rufiji ambapo ni nyumbani k
Loading...
a mwanaume kwa ajili ya kuuguzwa huko.

Hata hivyo baada ya kupata nafuu walirudi mjini kuendelea na shughuli zao, ndugu  huyu anasema kuwa hivi karibuni walikwenda kuwaangalia hali zao wakiwa huko gerezani na ndipo walipowakuta wameanza tena kudhofika sana.

Ndugu huyo anasema kuwa wamekuwa wakifanya mchakato kwa ajili ya kupata dhamna ili kunususru hali za ndugu zao.

Baada ya hapo waandishi wa habari walipata kuzungumza na kiongozi mmoja wa kituoni hapo na yeye alisema kuwa hajapata taarifa za ugonjwa wao lakini pia kama kweli ni wagonjwa basi kunataratibu huwa zinafuatwa na kupata matibabu lakini hawezi kutoa taarifa za mgonjwa au mahabusu.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE WAPO HOI GEREZANI AMBER RUTTY NA MPENZI WAKE WAPO HOI GEREZANI Reviewed by By News Reporter on 11/27/2018 06:41:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.