Loading...

YANGA YAENDELEA KUSUSIA UCHAGUZI

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Ally Mchungahela, amesema licha ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kutohudhuria kikao cha usaili wa wagombea, mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo unaendelea kama kawaida.

Juzi Kamati hiyo ya TFF iliendesha usaili kwa wagombea ambapo licha ya kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Yanga ya kuwaalika kwenye mkutano huo, hakuna kiongozi aliyehudhuria.

"Tuliendesha usaili wenyewe, tuliwapa taarifa ya kuwaomba wahudhurie lakini hawakutujibu wala hakuna aliyekuja, sisi tunaendelea na mchakato na uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa.., tutawaita tena kwenye kupitia mapingamizi,
Loading...
tunaamini watahudhuria," alisema Mchungahela.

Aliongeza kuwa hata kama viongozi wa Yanga hawatahudhuria katika vikao hivyo, mchakato wa uchaguzi utaendelea kama ilivyopangwa na watausimamia kwa kutumia katiba ya klabu hiyo ili kupata viongozi wapya.

Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13 mwakani jijini Dar es Salaam ili kujaza nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ambao walitangaza kujiuzulu.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia maagizo yaliyotolewa na serikali kupitia kwa Baraza la Mchezo la Taifa (BMT)baada ya klabu hiyo kupitisha muda mrefu bila kufanya uchaguzi wake.
Na Geofrey Okechi



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
YANGA YAENDELEA KUSUSIA UCHAGUZI YANGA YAENDELEA KUSUSIA UCHAGUZI Reviewed by By News Reporter on 11/27/2018 07:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.