Loading...

MSANII USHER RAYMOND ATESWA NA MAGONJWA YA ZINAA

Loading...
Baada ya kumalizana na mwanadada Quantasia Thompson, Usher Raymond bado anapambana na shtaka lingine la kumuambukiza ugonjwa wa zinaa mwanadada Laura Helm.

Sasa kwa mujibu wa mtandao wa Bossip umeripoti kuwa, Usher anataka taarifa zote juu ya kesi hiyo zibaki kuwa siri ya mahakama na wao wawili tu. Hivyo ameiomba mahakama ombi maalum (A gag order) la kuzuia taarifa za vipimo vyao na kila kitu zisitoke kwenye vyombo vya habari.

Usher hataki kuwafaidisha waandishi wa habari, hivyo lengo lake ni kulinda brand yake dhidi ya uharibifu wowote pia kuepuka kudhalilika baina yake na Laura.

Usher bado anakanusha tuhuma hizo huku Laura akimshtaki kwa makosa matatu: Uzembe, kumsababishia athari kama mawazo na kupelekea kuzorota kwa afya yake pamoja na kosa la udanganyifu.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MSANII USHER RAYMOND ATESWA NA MAGONJWA YA ZINAA MSANII USHER RAYMOND ATESWA NA MAGONJWA YA ZINAA Reviewed by By News Reporter on 11/02/2018 07:10:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.