Loading...

MTANZANIA MWINGINE AKABIDHIWA TUZO UJERUMANI

Mwanaharakati wa mazingira Gerald Bugurube kutoka Tanzania amekabidhiwa tuzo ya Ujerumani kutokana na juhudi zake za kutunza maliasili za nchi yake

Kwa miaka 44, Gerald Bigurube, Mtanzania mwenye umri wa miaka 66 amejitolea maisha yake kuwaokoa wanyama wa porini pamoja na mazingira asilia nchini mwake. 

Kwa muda mrefu amekuwa mkuu wa Mamlaka ya hifadhi za  Taifa za Wanyama pori Tanzania, TANAPA aliongoza mapambano dhidi ya majangili, na alianzisha juhudi za ujirani mwema baina ya mamlaka za kuhifadhi wanyamapori na jamii zina
Loading...
oishi karibu na mbuga, pamoja na utalii ambao ni mojawapo ya nguzo muhimu za uchumi wa Tanzania.

Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika (German Africa Award) inayotolewa kila mwaka kwa watu walioonyesha mfano katika sekta ya kutunza mazingira, mwaka huu imemwendea Gerald Bigurube kutoka Tanzania na na mwingine ni Clovis Razafimalala wa Madagascar. Watu hao wawili wamesifiwa kwa kujitolea kunusuru maliasili katika nchi zao. 

Wanaharakati hao wa mazingira walikabidhiwa tuzo hiyo Jumatatu 26.11.2018 nchini Ujerumani.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MTANZANIA MWINGINE AKABIDHIWA TUZO UJERUMANI MTANZANIA MWINGINE AKABIDHIWA TUZO UJERUMANI Reviewed by By News Reporter on 11/28/2018 07:01:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.