Loading...

NDOA NYINGI HATARINI KUVUNJIKA KISA VICOBA

Loading...
WANAWAKE wengi wanaochukua mikopo kwenye vikundi vya Vicoba bila kuwashirikisha wanandoa wenzao, wako hatarini kuachika au ndoa zao kuingia katika migogoro kutokana na usiri walio nao wakati wa kukopa fedha.

Sababu za hatari ya kuvunjika ndoa hizo ni kutokana na kukopa bila malengo, kuweka dhamana zisizo za kweli na wanafamilia moja kuwa kwenye kikundi kimoja cha vicoba.

"Unakuta idadi kubwa ya wanandoa wamekuwa wakiweka dhamana ya kama vile kiwanja, huku wakijua wazi kwamba kiwanja hicho ni mali ya mume wake na kwamba wakati anapofanya hivyo, mume wake anakuwa hana taarifa," aliyasema mkuu wa Vicoba mkoani Singida, Happy Lyimo juzi wakati wa ufunguzi wa kongamano la siku moja kwa vikundi vya kuweka na kukopa vya Manispaa ya Singida.

Aliongezea, wanachama wengi wa Vicoba wamekuwa wakikopa huku wakiwa hawana malengo na wakati mwingine wanakuwa wamekopa zaidi ya asasi moja ya mikopo kama vile Brac, Pride, Vicoba na sehemu zingine.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
NDOA NYINGI HATARINI KUVUNJIKA KISA VICOBA NDOA NYINGI HATARINI KUVUNJIKA KISA VICOBA Reviewed by By News Reporter on 11/29/2018 08:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.