Loading...

KENYA: RAIA WAWILI WA KOREA WAKAMATWA NA PESA BANDIA

Loading...
Raia wawili wa Korea Kusini washtakiwa kwa kumiliki pesa bandia milioni 700 za pauni na yuro.

Kim kyurak na Lee Ug walikutwa na fedha hizo katika ghorofa moja walilopanga huko Kilimani, Kenya mnamo Novemba 19.

Walifikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkuu Francis Andayi.

Mashtaka dhidi yao yalisomwa kwamba walikamatwa na makaratasi waliyotaka kuyagushi na kufananisha na pesa halisia za sasa.

Baadhi ya nakala 10,000 za noti bandia za Euro (yuro), zenye thamani ya zaidi milioni 26 pesa za Tanzania zilikamatwa katika nyumba yao.

Wawili hao wakamatwa na zaidi ya pauni 1,200 (sawa na Sh. milioni 7)

Toka jana walilazwa selo leo ndio hukumu yao itasomwa.
Na Hamisi Ramadhan.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KENYA: RAIA WAWILI WA KOREA WAKAMATWA NA PESA BANDIA KENYA: RAIA WAWILI WA KOREA WAKAMATWA NA PESA BANDIA Reviewed by By News Reporter on 11/28/2018 08:25:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.