Loading...

JPM AMTUMA LOWASSA, AMUITA 'SUPERMAN'

RAIS Dk. John Magufuli jana amemmwagia sifa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kwa kumwita shujaa na kumtaka akawashauri viongozi wenzake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wafuate sheria vinginevyo wataishia gerezani.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), iliyojengwa kwa Dola za Marekani milioni 41.28 (sawa na Sh. bilioni 93).

Kadhalika, Rais Magufuli alimpongeza Lowassa kwa uamuzi wake wa kuhudhuria shughuli ya ufunguzi wa maktaba
Loading...
iyo tofauti na viongozi wengine wa upinzani ambao hawakufika.

"Sikushangaa kumuona Lowassa kuwa hapa ingawa kwa miaka mingi hatujaonana katika hafla mbalimbali, nakupogeza sana Lowassa, kwanza kwa  utulivu wako wewe ndiye tuligombea urais, lakini nilipokutupa chini ukaenda ukapumzika mzee wa watu vizuri, wenye kelele wengine hawakugombea," alisema Rais Magufuli na kuongeza:


"Wewe ukatulia mzee wangu ukijua kwenye mashindano yoyote kuna kushinda na kushindwa, mimi ninakupongeza kwa moyo wako wa kizalendo na wa kitanzania na hili ninalisema kwa dhati, tunahitaji watu waliokomaa kwenye vyama mbalimbali kama wewe, wewe ni Superman (shujaa)".
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JPM AMTUMA LOWASSA, AMUITA 'SUPERMAN' JPM AMTUMA LOWASSA, AMUITA 'SUPERMAN' Reviewed by By News Reporter on 11/28/2018 07:38:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.