Loading...

RUBANI KUCHUNGUZWA BAADA YA KULALA AKIWA ANGANI

Loading...
Rubani mmoja nchini Australia anafanyiwa uchunguzi baada ya kushikwa na usingizi alipokuwa akiendesha ndege ya aina ya Piper PA-31 ya shirika la Vortex Air Novemba 8, 2018.

Imeripotiwa kuwa ndege hiyo ilipaa umbali wa takriban kilomita 50 kutoka kwenye uwanja wa ndege ilikostahili kutua. 

Kulingana na taarifa za CNN, ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Devonport kwenda King Island huko Tasmania iliweza kutua salama baada ya dereva kuamka na kugundua kwamba alikuwa amepita uwanja alikotakiwa kutua.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Vortex Air Colin Tucker alisema dereva huyo alilala makusudu akiendesha ndege hiyo. 

"Wataalamu wa kudhibiti ndege angani hawakuweza kuwasiliana na rubani huyo walipogundua kwamba ndege hiyo ilikuwa imepita uwanja iliyotarajiwa kutua, huenda rubani aliweka ndege hiyo katika hali ya kujiendesha yenyewe, hadi sasa haijaeleweka jinsi alivyofanikiwa kuamka usingizini na kutua salama," Tucker alisema.

Aidha, ilibainika kwamba rubani huyo alikuwa mapumzikoni na hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuendesha ndege aliporejea kazini.

Mamlaka ya usafiri nchini humo ilisema itamhoji rubani huyo kwa kina na kuchunguza mipangilio ya huduma za shirika hilo kabla ya kutoa ripoti kamili.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RUBANI KUCHUNGUZWA BAADA YA KULALA AKIWA ANGANI RUBANI KUCHUNGUZWA BAADA YA KULALA AKIWA ANGANI Reviewed by By News Reporter on 11/29/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.