Loading...

MCHUNGAJI AINGIA MITINI BAADA YA KUVAMIWA NA MCHEPUKO MADHABAUNI

Loading...
KENYA. Kimetokea kisa kimoja na filamu za kuigiza baada ya aliyedaiwa kuwa ni mchepuka wa pasta kumfuata mchungaji huyo hadi madhabauni wakati ibadi imepamba moto.

Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la Taifa Leo, mchungaji huyo alisongwa na mawazo na kujawa na wasiwasi punde tu baaada ya kumuona mwanadada huyo akiingia kanisani na kuketi katika viti vya nyuma.

Inadaiwa kuwa mchungaji na kimada huyo walikuwa pamoja usiku wa kuamkia siku ya ibada wakistarehe na hivyo pasta alipomuona akiingia kanisani bila kumpasha habari, alijua fika kuwa huenda kimada huyo angemtoa nishai hadharani.

Pasta huyo alitoka madhabahuni akijifanya kupokea simu na aliporudi ndani, alimuomba pasta mwenzake kushika usukani akidai kuwa alipata jambo la dharura nyumbani na alitakikana kufika upesi.

Baadhi ya washiriki wa kanisa hilo walianza kunong'onezana kwa sauti za chini chini maana walipata fununu kuhusu uhusiano uliopo kati ya wawili hao.

''Mchungaji amepata jambo la dharura nyumbani kwake. Kwa hivyo anahitaji maombi yetu,’’ naibu wake alisema.

Haikubainika kilichojiri baada ya pasta huyo kuondoka.
Na Bashir Hashim.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MCHUNGAJI AINGIA MITINI BAADA YA KUVAMIWA NA MCHEPUKO MADHABAUNI MCHUNGAJI AINGIA MITINI BAADA YA KUVAMIWA NA MCHEPUKO MADHABAUNI Reviewed by By News Reporter on 11/29/2018 09:57:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.