Loading...
Ni takribani miaka miwili sasa tangu mwimbaji Saida Karoli arudi kutumbuiza katika majukwaa makubwa kama Sauti za Busara. Mwimbaji huyo anatarajiwa kutumbuiza katika maeneo ya Nairobi na Kisumu nchini Kenya, kuanzia wiki ijayo.
Shoo hizo mbili zilizopewa jina la "African Music Extravaganza," zimeandaliwa na kampuni ya Melamini Promotion Ltd, na itashirikisha wasanii kutoka Kenya, Tanzania na Congo.
Akiongea akiwa Mkoani Mbeya Saida alisema atafurahi kwenda Kenya baada ya muda kipindi kirefu, "Kila kitu kipo sawa, mara ya mwisho kwenda kule ilikuwa poa sana na nina hamu ya kutumbuiza tena," alisema. Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni "Mapenzi Kizunguzungu", "Maria Salome", na "Kitobero".
Ijapokuwa, Maria Salome ndio ilifungua mlango wa yeye kurudi tena kwenye gemu la muziki.
Ilimpa kiki baada ya mwanamuziki Diamond Platinumz kuirudia nyimbo ya salome, japo mengi yalizungumzwa hasa katika upande wa maslahi yake.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

SAIDA KAROLI KUFANYA 'TOUR' KUBWA YA MUZIKI KENYA
Reviewed by By News Reporter
on
11/30/2018 09:31:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: