Loading...
Dawa mpya ya kupanga uzazi imegunduliwa huko Marekani tayari kwa majaribio. Kwa Afrika Mashariki, Kenya ni miongoni mwa nchi saba ambazo zimechaguliwa ambapodawa hiyo ya kupanga uzazi kwa wanaume itajaribiwa.
Dawa hiyo ambayo ipo kwa mfumo wa jeli ambayo wanaume wanatarajiwa kupaka katika uume wao kila siku ni kujaribu kuwapa vijiti wanaume pia ili kushiriki kikamilifu kupanga uzazi kwa njia nyingine ukiacha kutumia mipira (kondomu).
Kwa mujibu wa Komonews.com, mbinu hiyo haitatumika kukinga maradhi ya zinaa kama ilivyo kondomu.
Chuo Kikuu cha Washington tayari kimeanza kuwasajili wanandoa kwa majaribio hayo.
Kulingana na wasomi wa chuo hicho, jeli hiyo inatarajiwa kupunguza mbegu za uzazi na sio kupunguza hamu ya tendo la ndoa.
Inadaiwa zaidi ya asilimia 40 za ujauzito duniani hazikupangwa.
Zaidi ya wanandoa 400 wanatarajiwa kujumuishwa katika awamu ya kwanza yajaribio hilo kwa matumizi ya jeli hiyo ya Nesterone.
Na Catherine Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAUME KUANZA KUPANGA UZAZI, DAWA ZAFANYIWA MAJARIBIO
Reviewed by By News Reporter
on
11/30/2018 08:22:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: