Loading...

WANAFUNZI WAWILI WAFARIKI KWA KUPIGA 'SELFIE'

Loading...
Wanafunzi wawili mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jaromogi Oginga Odinga (JOOUST) na Taasisi ya Mafunzi ya Ufundi ya Bondo walizama maji katika Mto Yala, Jumamosi, Novemba 3. 

Taarifa zinataarifa kwamba, Derrick Auka, mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa JOOUST na Sharlet Atieno, walikuwa wamekwenda matanuzi kabla ya mauti hayo kuwakumba.

Akithibitisha kutokea mkasa huo, Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Jaramogi Stephen Agong' alisema wawili hao walikufa maji wakipiga picha za ‘selfie’. 

"Inasikitishasana. Wanafunzi wawili mwanamume mmoja kutoka Jaramogi na msichana wa Bondo Technical, walikuwa wakipiga picha za ‘selfie’ kando kando mwa mto kabla ya mkasa huo kuwapata," Agong' alisema.
Na Hamadi Nalimi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAFUNZI WAWILI WAFARIKI KWA KUPIGA 'SELFIE' WANAFUNZI WAWILI WAFARIKI KWA KUPIGA 'SELFIE' Reviewed by By News Reporter on 11/06/2018 04:20:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.