Loading...

MAMA KANUMBA: SIMCHUKII LULU KAMA WATU WANAVYODHANI

Loading...
Mama wa marehemu Steven Kanumba amefunguka na kusisitiza kuwa katika maisha yake hajawahi kumchukia msanii Lulu Michael kama ambavyo imekuwa ikisikika masikioni kwa watu na watu wengi kuamini hivyo kwa sababu ya kumuua mtoto wake.

Mama huyo anasema kuwa hajawahi kumchukia Lulu lakini amekuwa na uchungu kila siku kwa sababu Kanumba kifo chake kimesababishwa na mtu mwingine.

Mama kanumba alipokuwa akiongea na EATV, anasema  “kanumba ni mwanangu na nilikuwa ninampenda sana na ukizngatia nilimlea kwa tabu sana lakini anatokea mtu anamuua, mimi simchukuii lulu mimi ninampenda sana, ninamtakia kila lenye kheri katika maisha yake.

Kama bado kuna kumbukumbu, mama kanumba na lulu walikuwa marafiki sana hasa baada ya kifo cha kanumba lakini baada ya hapo mahusiano yao yalianza kufa na hata kufikia hatua ya kuwa maadui wakubwa.

Mama huyo ukiachana na kulalamika  katika mitandaokuwa lulu amekuwa hamuheshimu wala kumsaidia lakini alichukizwa sana na hukumu aliyopewa mwanadada huyo ikiwa kama adhabu ya kifo cha msanii huyo ambae alikuwa katika mahusiano  na Kanumba.
Na Neema Joshua.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
MAMA KANUMBA: SIMCHUKII LULU KAMA WATU WANAVYODHANI MAMA KANUMBA: SIMCHUKII LULU KAMA WATU WANAVYODHANI Reviewed by By News Reporter on 11/06/2018 07:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.