Loading...

CHANZO CHA SHEREHE YA MWAKA MPYA

Loading...
Wazo la kutumia au kuienzi tarehe 1 Januari kama siku ya kwanza ya mwaka mpya ilianza katika utawala wa Julian Caesar, miongo mitano (5) kabla ya kuzaliwa kwa Yesu huko Uyahudini.

Kalenda nyingi zilizotumika kabla ya utawala wa Caesar zilitengenezwa na Julian Kalenda miaka 46 B.C.(kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), lakini alitaja Januari 1 kama siku rasmi ya kufungua mwaka mpya. Hiyo ilikuwa siku rasmi ya viongozi wakubwa wa serikali ya Roma, kuingia ofisi kwa ajili ya kuutumikia umma katika kipindi chote cha utawala wao.

Ijapokuwa kalenda ya Julian ilifanikiwa kusambaa na kupata umaarufu, baadhi ya maeneo waliendelea kutumia tarehe za mwezi Machi na Septemba kama siku za mwaka mpya. Katika maeneo ya Ulaya, kwa mfano, sherehe za mwaka mpya utazamwa kama sherehe za wapagani, kwahiyo sikukuu iliamishwa kulingana na tarehe zilizopendekezwa, ikiwemo Disemba 25, siku ambayo makanisa ya Kikristo kuabudu na kusherehekea kama kuzaliwa kwa Yesu, na Machi 25.

Mnamo mwaka 1570, Papa Gregory alizindua kalenda ya Wagregory, na kuirudisha tena Januari 1, kama siku ya kusherehekea mwaka mpya na mabadiliko hayo hayakuwekwa katika mchakato huko England mpaka ilipofika mwaka 1752. Mpaka kufikia mwaka huo na huko nyuma Waingereza, Wamarekani na makoloni yao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya mwaka mpya Machi 25.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
CHANZO CHA SHEREHE YA MWAKA MPYA CHANZO CHA SHEREHE YA MWAKA MPYA Reviewed by By News Reporter on 12/31/2018 02:32:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.