Loading...
Unapoendelea kusherekea kipindi hiki muhimu cha sikukuu naomba nikukumbushe zoezi moja muhimu katika maisha yako. Zoezi hili ukilifanya kwa umakini na kwa usahihi kama inavyotakiwa kuwa ni wazi kwamba mwaka 2019 utakuwa na tofauti kubwa na miaka mingine katika maisha yako.
Kwa mfano, ulishawahi kujiuliza kwa nini ukifanya maamuzi ya kununua aina fulani ya gari ghafla utashangaa barabarani unaanza kuziona gari za aina hiyo kwa wingi tofauti na jinsi ilivyokuwa awali ? Hii huwa inatokea kwa sababu akili zetu hufanya kazi kwa ufanisi mkubwa pale tunapokuwa tumebainisha kwa uwazi nini tunataka, katika mazingira haya akili yako itakuonesha na kukukutanisha na kila kitu ambacho kinaendana na kile unachokitaka.
Mfano huu ni katika kufafanua zoezi hili muhimu, kabla ya mwaka mpya kuanza HAKIKISHA UNATAMBUA NA KUBAINISHA NINI UNATAKA KATIKA MAISHA YAKO. Usiwe njia panda katika hili, usiwe katika hali ya kutokuwa na uhakika juu ya kile unachotaka, usianze mwaka bila kujua unataka nini katika maisha. Weka bayana jambo hili ili AKILI yako pia iweze kutambua unataka nini na ikusaidie.
Uwezo wa akili ya mwanadamu ni wa ajabu sana, akili ikitambua unataka nini itakukutanisha na watu muhimu kukusaidia kufanikisha kile unachokitaka, itakuonesha fursa nyingi juu ya jambo hilo, itakupeleka sehemu muhimu, itakuonesha kila kitu ambacho unatakiwa kukiona ili ufanikishe kile unachotaka. Yote haya ni kwa sababu inatambua unataka nini.
Kama hili halijakutokea jichunguze huenda hueleweki, hauko bayana na unaichanganya akili yako juu ya nini unataka kiasi cha kujikuta inashindwa kufanya kazi.
'Mabadiliko ni sasa na wakati ndio huu'.
Na Haika Gabriel.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

KABLA YA KUINGIA 2019, UNAPASWA KUTAMBUA KITU HIKI
Reviewed by By News Reporter
on
12/31/2018 03:15:00 PM
Rating:

Hakuna maoni: