Loading...

KONTENA LA JOKATE KUPIGWA MNADA NA TRA??

Loading...
Kontena  lililosheni nywele bandia, mali ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwengelo lipo hatarini kupigwa mnada baada ya kukwama kulipia ushuru bandarini.

Kwa mujibu wa Tangazo la Kamishna wa Forodha na Ushuru, Usaje Asubisye la Desemba 18, ametoa Ilani ya kusudio la kupiga mnada kwa kontena hilo na ya vigogo wengine kwa kushindwa kulipia ushuru hadi siku ya tangazo.

Jokate aliingiza kontena hilo namba HJCU2320135 kupitia kampuni yake ya Kidot ambayo inajishughulisha na mambo ya mitindo na urembo.

Hata hivyo, Jokate alipotafutwa  alimtaka Mwandishi  kuwasiliana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidot, aliyemtaja kwa jina moja la Bruce, lakini alipotafutwa na kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (SMS), hakuweza kujibu licha ya ujumbe huo kumfikia.

Mbali ya Mkuu huyo wa Wilaya, yapo Makontena mengine ya vigogo na taasisi mbalimbali ambayo yamepewa siku 30 kulipia ushuru vinginevyo yatapigwa mnada.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KONTENA LA JOKATE KUPIGWA MNADA NA TRA?? KONTENA LA JOKATE KUPIGWA MNADA NA TRA?? Reviewed by By News Reporter on 12/28/2018 05:49:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.