Loading...

RAPA MKONGWE DMX KUACHILIWA HURU MWEZI UJAO

Loading...
Rapa DMX wa nchini Marekani ambaye ni nguli wa muziki wa HipHop, anatarajiwa kuachiwa huru mwezi ujao.

Mwanasheria wa rapa huyo, Murray Richman, aliiambia mtandao wa TMZ kwamba msanii huyo wa Marekani ataachiliwa huru kutoka katika Taasisi ya Mafunzo ya Gilmer mnamo tarehe 27 Januari mwakani, na anafurahi kurudi nyumbani kwenye familia yake na yuko tayari kwa kuendelea na kazi yake ya muziki na uigizaji baada ya kutumikia kifungo cha miezi 12 jela kwa ukwepaji wa kodi.

DMX, ambaye ana watoto 15, ameandika nyimbo nyingi akiwa jela na amepanga kuziachia katika albamu yake mpya, kulingana na TMZ.
Na George Okechi.


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RAPA MKONGWE DMX KUACHILIWA HURU MWEZI UJAO RAPA MKONGWE DMX KUACHILIWA HURU MWEZI UJAO Reviewed by By News Reporter on 12/28/2018 06:02:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.