Loading...
Inawezekana uliweka lengo fulani na kwa sasa umefanikiwa kukamilisha lengo hilo. Ulikusidia kupata kiwango fulani cha elimu na umekipata, ulipanga kufikisha kiwango fulani cha pesa na umefikia, uliazimia kupata nafasi fulani katika ajira yako na umeipata. Baada ya hapo nini kinaendelea?
Kuna kosa moja ambalo watu wengi wamejikuta wakilifanya pengine bila kujua, kosa hili ni kuweka nanga baada ya kufikia mafanikio fulani ambayo walitamani kuyafikia. Wametosheka na hali ama hatua waliyofikia. Hali ni tofauti kwa watu wenye mafanikio makubwa na wanaoendelea kufanikiwa , wanatambua mtego huu na wamefanikiwa kuukwepa.
Ukiona umefikia hatua ya kutosheka na hatua uliyonayo au jinsi ulivyo wewe kama wewe basi tambua kwamba uko katika ukanda wa hatari, unakoelekea si kuzuri.
Unapaswa kila siku kuwa zaidi ya jana, ukiona mafanikio yako ya jana bado ni makubwa basi tambua leo kuna jambo unatakiwa kufanya zaidi. Unatakiwa kukua kila siku katika nyanja zote, kujifunza vitu vipya kila siku, kujaribu mambo mapya kila siku na kukutana na changamoto mpya kila siku.
Ukifanikisha jambo moja iwe ni hatua ya kwenda mbali zaidi kwa kuboresha zaidi. Usikae na kuweka kambi kuwa umefika
Na Vicent Stephen.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NINI UNAPASWA KUFANYA BAADA YA KUTIMIZA LENGO ULILOJIWEKEA?
Reviewed by By News Reporter
on
12/12/2018 04:16:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: