Loading...

TAARIFA KWA UMMA: PICHA YA GARI LA BENKI YA TIB ILIYOBEBA MBUZI KWENYE GURUDUMU LA AKIBA

Loading...
Kumekuwa na picha inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha gari aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 yenye namba za usajili SU 38431 ikiwa imebeba mbuzi aliyefungwa kwenye gurudumu la akiba ambalo mfuniko wake una nembo ya Benki ya Maendeleo TIB.

Benki inapenda kukiri kuwa gari hilo ni mali ya Benki ya Maendeleo TIB. Dereva wa gari hiyo, aliyekuwa peke yake ndani ya gari, alikuwa akielekea Dar es Salaam kutokea Mwanza kwa safari ya kikazi siku ya ijumaa, tarehe 14 Disemba 2018.

Kitendo alichofanya dereva wa gari hilo hakikuwa ni maelekezo ya Benki na ni dhahiri kuwa amekiuka maadili ya kazi yake. Aidha, Benki inatambua kuwa kitendo hicho kimeenda kinyume na matumizi kinyume na matumizi sahihi ya mali za Umma, haki za wanyama, pamoja na kanuni za usalama barabarani.

Benki inaendele kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya dereva husika ili kurejesha nidhamu na maadili kazini; na pia kuwa fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hiyo.

Benki inatoa shukrani zake za dhati kwa raia mwema aliyetoa taarifa za tukio hili ambalo limeifedhehesha Benki ya Umma. Tunatoa rai kwa Umma kuendelea kutoa taarifa kuhusu matukio yanayokiuka sheria, miongozo na taratibu zilizowekwa. Hii itawezesha kurejesha nidhamu na uadilifu katika jamii yetu.

Imotolewa na:
Mkurugenzi Mtendaji
Benki ya Maendeleo TIB
Building No. 3, Mlimani City Office Park; Sam Nujoma Road
PO Box 9373, Dar Es Salaam


Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
TAARIFA KWA UMMA: PICHA YA GARI LA BENKI YA TIB ILIYOBEBA MBUZI KWENYE GURUDUMU LA AKIBA TAARIFA KWA UMMA: PICHA YA GARI LA BENKI YA TIB ILIYOBEBA MBUZI KWENYE GURUDUMU LA AKIBA Reviewed by By News Reporter on 12/15/2018 09:53:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.