Loading...

VIGOGO WA TANESCO KUTUMBULIWA BAADA YA UMEME KUKATIKA

Loading...
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuwavua nyadhifa zao manaibu Wakurugenzi wa sekta ya uzalishaji na usambazaji wa Shirika la umeme nchini (TANESCO) kutokana na uzembe uliojitokeza kwenye gridi ya taifa na kusababisha umeme kukatika mara nne kwa kipindi cha miezi miwili nchi nzima.

Katika kikao cha dharura alichoitisha leo tarehe 16 Disemba, 2018 ambapo alizungumza moja kwa moja pamoja na waandishi wa habari, aidha waziri alisema uzembe huo ulianza kujitokeza mnamo tarehe 28 Novemba, saa 9 usiku na kuchukua dakika 30 mpaka kurudi tena kwa nchi nzima na ilisababishwa na gridi kutoka.

"Lakini Novemba 30 pia saa 12 gridi ilitoweka na maeneo mengi mbali mbali yalikosa umeme, tarehe 4 Novemba pia umeme ulitoweka kwa kusababishwa na gridi kutoweka ila tukaitana hapa na kukubaliana kuwa baada ya siku nne hilo tatizo litatoweka lakini halikuzaa mafanikio," akitoa maelezo ya kilichotokea kwa uzembe huo.

Aliendelea Kusema: "Mpaka jana kufikia saa 10.30 jioni mpaka takribani saa 12 hadi 1 usiku umeme pia gridi ilitoka na kusababisha maeneo mengi ya nchi yetu nayo kukosa umeme, sasa hali hii imetokea mara nne ndani ya miezi hii miwili na wakati nchi ina ziada ya umeme."

Akiongea mbele ya Mwenye wa bodi na waandishi wa habari Mhe. Waziri alisema nchi ina ziada ya umeme ya wastani wa megawati 252 kwahiyo hakuona sababu ya wanachi kukosa umeme ikiwa nchi ina ziada ya umeme.

Akitoa maelekezo katika bodi nini wanapaswa kufanya ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo, Mheshimiwa Waziri aliiagiza bodi hiyo kuunda timu mahususi kwa ajili ya kufuatilia na kupata majawabu kinachosababisha hayo yote kutokea na ndani ya siku saba anataka majibu.

Akiendelea kuwaambia bodi husika nini cha kufanya alisema: "Jambo hili linapotokea manake kuna uzembe katika usimamizi ama kuna kutokufuatilia maelekezo ya serikali au kunaweza kukawa na hujuma katika watumishi wasio wazalendo kwahiyo kuanzia sasa bodi ichukue hatua za kinidhamu ikiwemo kuwavua nyadhifa zao manaibu Wakurugenzi wa sekta ya uzalishaji na usambazaji wa Shirika."
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
VIGOGO WA TANESCO KUTUMBULIWA BAADA YA UMEME KUKATIKA VIGOGO WA TANESCO KUTUMBULIWA BAADA YA UMEME KUKATIKA Reviewed by By News Reporter on 12/16/2018 05:55:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.