Loading...
Klabu ya Chelsea Jumatano usiku imekubali kipigo kizito cha goli nne bila majibu kutoka kwa klabu ya Bournemouth.
Kipigo hicho ni kikubwa zaidi kwa Chelsea kwa kipindi cha miaka 23 kwenye Ligi ya Premia. Kipigo kikubwa cha 'mbwa koko' ambacho Chelsea ilipokea ilikuwa Septemba 1996 walipofungwa 5-1 dhidi ya Liverpool.
Mpaka mapumziko kulikwa hakuna goli lililofungwa. Kipa wa Bournemouth Artur Boruc alikuwa nyota wa mchezo katika kipindi cha kwanza kwa kuzuia nafasi za wazi tano za Chelsea.
Gharika langoni mwa Chelsea ilianza dakika mbili tu baada ya mapumziko kwa Joshua King kuandika goli la kwanza katitika dakika ya 47.
Kipigo hicho kimewashusha Chelsea mpaka nafasi ya tano wakiwa sawa na Arsenal kwa alama 47 lakini Gunners wapo nafasi ya nne kwa kuwa wamefunga magoli mengi kuliko Blues.
Ushindi wa Bournemouth unaifaya klabu hiyo kupaa mpaka nafasi ya 10 kwenye msimao wa ligi na kufikisha alama 33.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

CHELSEA WASHUSHIWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Reviewed by By News Reporter
on
1/31/2019 11:02:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: