Loading...

CHRIS BROWN AKAMATWA UFARANSA KWA MADAI YA UBAKAJI

Loading...
Mwanamuziki nyota kutoka Marekani Chris Brown amekamatwa akiwa Paris nchini Ufaransa baada ya kipusa mwenye umri wa miaka 24 kumkashifu kwa madai ya ubakaji.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na maafisa wa polisi, kimada huyo alidai Chris alikuwa akiishi katika hoteli ya Le Mandarin Oriental ambapo alitaka kumbaka kati ya usiku wa Jumanne Januari 15 na Jumatano 16.

Mwanamuziki huyo alikuwa nchini Ufaransa kuhudhuria tamasha la wanamitindo. Chris anasemekana alikutana na kimada huyo ambaye hajatajwa kwa majina katika klabu ya Le Crystal na baadaye kuongozana naye hadi kwenye chumba alimokuwa akilala mwanamuziki huyo.

Kimada huyo alikuwa akistarehe na wenzake wawili kabla ya Chris kumtaka waende naye kwenye chumba chake cha kulala na hapo ndipo alitaka kumbaka.

Tayari maafisa wa polisi nchini humo wamewakamata watu watatu wanaosemekana walikuwa na Chris wakati kitendo hicho kilipotendeka.

"Chris alikamatwa na wenzake wawili Jumatatu, uchunguzi dhidi yake unaendelea. Aliripotiwa kutekeleza kitendo hicho Jumatatu Januari 15, 2018," Ripoti ya polisi ilisoma.

Mwanamuziki huyo amekumbana na mkono wa sheria mara kadhaa kwa muda wa miaka 10 kwa makosa ya hapa na pale yakiwemo yale aliyoshtakiwa kwa kumdhulumu mpenzi wake Rihana mnamo mwaka 2009.
Na Said Hussein.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
CHRIS BROWN AKAMATWA UFARANSA KWA MADAI YA UBAKAJI CHRIS BROWN AKAMATWA UFARANSA KWA MADAI YA UBAKAJI Reviewed by By News Reporter on 1/23/2019 10:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.