Loading...

WATU 14 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MGODI WA DHAHABU NCHINI RWANDA

Loading...
Wafanyakazi 14 wamepoteza maisha yao katika mgodi wa dhahabu katika mkoa wa Mwulire nchini Rwanda, Afrika ya Mashariki.

Jean Claude Rwagasana, afisa wa wilaya ya Mwulire, amesema kuwa hivi karibuni kumekuwa na majanga tofauti katika mgodi wa dhahabu kutokana na mvua nyingi katika eneo hilo.

"Watu 14 wamepoteza maisha wakiwemo wanawake 7. Kwa bahati mbaya, timu ya uokoaji haikufanikiwa kuokoa hata mtu mmoja", alisema Rwagasana.

Ajali kama hiyo ilitokea mwaka 2017 na kusababisha vifo vya watu 27.
Na Geofrey Okechi.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WATU 14 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MGODI WA DHAHABU NCHINI RWANDA WATU 14 WAPOTEZA MAISHA KATIKA MGODI WA DHAHABU NCHINI RWANDA Reviewed by By News Reporter on 1/23/2019 10:06:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.