Loading...
Ndege kutoka katika mji wa Surgut kuelekea Moscow imelazimika kutua kwa dharura Magharibi mwa Siberia kutokana na kutekwa nyara na mtu mmoja mwenye silaha nchini Urusi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Urusi, abiria huyo alipanda ndege hiyo SU1515 akiwa na nia ya kuelekea nchini Afghanistan kwa kupitia mjini Moscow. Ndipo baadaye akajaribu kutekeleza utekaji huo.
Taarifa za awali za hapo jana jumanne pia ziling'amua kuwa mtu huyo alikuwa ni mlevi. Alijifanya ameumia na kufanikiwa kuingia katika chumba cha marubani kwa madai kuwa alienda kupatiwa msaada na kuamuru ndege hiyo itue mahali ambako haikustahili kutua ndege hiyo.
Ndege hiyo iliyokuwa inapaswa kutua katika uwanja wa ndege Sheremetyevo mjini Moscow ililazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Hanty-Mansiysk.
Baadeye walikuja wahudumu wa ndege wanaohusika na maswala ya ulinzi na kumkamata. Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala uharibifu wowote wa mali uliotokea.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MLEVI ALIVYOJARIBU KUTEKA NYARA NDEGE NCHINI URUSI
Reviewed by By News Reporter
on
1/23/2019 09:47:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: