Loading...

WAUMINI WA KANISA KATOLIKI KOTE DUNIANI KUOMBA NA PAPA MTAKATIFU ANA KWA ANA KUPITIA SIMU

Loading...
Kanisa Katoliki limezindua teknolojia mpya itakayowawezesha waumini wake kote ulimwenguni kuomba pamoja na Papa Mtakatifu Francis bila ya kulazimika kwenda Vatican.

Haya yamejiri mapema baada ya Papa Francis kukiri hana ufahamu wa teknolojia ya kisasa lakini amepongeza maendeleo hayo mapya.

Teknolojia hiyo ya app (programu tekelezi) kwa jina ‘Click to Pray’, ilizinduliwa Jumapili, Januari 20, wakati wa misa iliyofanyika St Peter’s Square, jijini Vatican. 

Teknolojia hiyo chini ya mtandao wa Katoliki wa Maombi ya Pamoja na Papa, itawafahamisha mapema waumini kufahamu anachoombea Papa na kuungana naye katika maombi kuhusu masuala mbalimbali duniani kwa mfano kuwaombea amani na utulivu kwa waathirika wa ugaidi.

"Click to Pray itasaidia waumini duniani kuungana na Papa katika maombi," taarifa ya www.clicktopray.org ilisema.

Papa Francis huwaongoza zaidi ya waumini 1.3 bilioni wa Kanisa Katoliki ulimwenguni na kwa sababu ya teknolojia mpya, wataweza kufuatilia na hata kuomba pamoja naye kila siku.

Aliwataka waumini kote ulimwenguni kuwaombea waathirika 170 waliozama katika Bahari ya Mediterranean baada ya boti mbili walizokuwa wakisafiria kutoka Morocco kwenda Libya kuzama katika mikasa tofauti Januari, 2019. 

"Moyo wangu upo na waathirika 170 waliozama Bahari ya Mediterranean. Walikuwa wakitafuta maisha bora na huenda wangekuwa waathirika wa ulanguzi wa watu. Tuwaombee na waliosababisha vifo vyao," alisema.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAUMINI WA KANISA KATOLIKI KOTE DUNIANI KUOMBA NA PAPA MTAKATIFU ANA KWA ANA KUPITIA SIMU WAUMINI WA KANISA KATOLIKI KOTE DUNIANI KUOMBA NA PAPA MTAKATIFU ANA KWA ANA KUPITIA SIMU Reviewed by By News Reporter on 1/23/2019 10:43:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.