Loading...
Waandamanaji wenye hasira kali wamefunga barabara kuu ya Gulu - Kampala wakitaka kujengwa kwa matuta.
Raia hao wenye hasira kali walianza maandamano hayo jumanne tarehe 22 Januari, 2019 muda wa saa tatu asubuhi baada ya ajali mbaya iliyotokea katika kituo cha biashara cha Koro Abili, kilometa 8 kutoka jiji la Gulu. Watu watatu waliumia vibaya katika ajali baada ya kuvunjika mikoni na kupata majeraha makubwa vichwani na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoani Gulu.
Wananchi hao waliojawa na hasira waliamua kubeba magogo na majabali makubwa ili kuziba barabara hiyo kwa lengo la kuilazimisha mamlaka kuwajengea matuta ili kupunguza ajali hizo.
Waandamanaji walilalama kuwa kutokuwepo kwa matatu kunasababishwa kupoteza uhai wa ndugu zao wengi kisa ajali.
Peter Mugabi, Kamanda wa polisi wa wilaya ya Omoro aliwasihi wananchi hao kutawanyika eneo hilo ili kuruhusu magari kuendelea na safari zake na kutoa vizuizi hivyo kwa kuwa dereva aliyehusika na ajali ameshatiwa mbaroni.
Na Daudi Kiseri.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

WAANDAMANAJI WAFUNGA BARABARA KUU YA KAMPALA
Reviewed by By News Reporter
on
1/23/2019 11:19:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: