Loading...

JE WAJUA NGULI WA RAGGAE 'BUJU BANTON' ALICHOMWAMBIA BOB WINE WAKIWA JAMAIKA?

Loading...
Hivi karibuni mwanamuziki wa raggae na Mbunge wa nchini Uganda, Bob Wine alifanya ziara yake huko Kingston - Jamaica kwenda kutumbuiza katika tamasha kubwa la raggae linalojulikana kwa jina la 'The Rebel Salute' - akiwa kama mtu wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushiriki kwenye tamasha hilo.

Ila ambacho ulikuwa haujui ni kwamba, mkongwe wa muziki wa raggae Buju alikutana na msanii huyo na kuzungumza machache na kati ya vitu walivyozungumza alimsisitiza kutoogopa kukaa jela kwa kile anachokiamini.

Kwa kuwa hata yeye alishawahi kukaa jela kwa muda wa miaka 7 kwa kosa ambalo hakutenda. Buju ameonekana kuwa mtu muhimu kwa Bob Wine kumrudisha katika mstari kwa kile alichokitazamia.
Na Daudi Shomari.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JE WAJUA NGULI WA RAGGAE 'BUJU BANTON' ALICHOMWAMBIA BOB WINE WAKIWA JAMAIKA? JE WAJUA NGULI WA RAGGAE 'BUJU BANTON' ALICHOMWAMBIA BOB WINE WAKIWA JAMAIKA? Reviewed by By News Reporter on 1/23/2019 11:46:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.