Loading...
Msanii wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameshaweka wazi kuwa anataka kumuoa Mpenzi Wake Tanasha Donna Oketh Lakini inadaiwa kikwazo ni tofauti za kidini.
Gazeti la Risasi Jumamosi linaripoti kuwa Diamond ni Muislam huku Tanasha akiwa ni Mkristo ambapo inaaminika kuwa lazima mmoja abadili dini kumfuata mwenzake.
Tanasha, akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa mashabiki kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, alisema kuwa kutokana na mipango ya ndoa inayofuata hawezi kukataa kuhamia Tanzania kwa sababu kwake kwa sasa ni nyumbani kwa pili.
Tanasha alisema kuwa, kuhamia kwake Tanzania haiwezi kuwa shida, lakini kwa suala la dini, hawezi kubadili dini. Tanasha alisema kuwa kila dini imekuwa ikimuamini Mungu mmoja hivyo hakuna sababu ya yeye kubadili dini zaidi ya kila mmoja kuheshimu dini ya mwingine.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa wanafamilia ya Mondi aliyefuatilia mjadala huo alisema kuwa, jambo hilo ni kikwazo kikubwa kwani wao kama familia walitarajia Tanasha angebadili dini ili kuungana na Mondi ambaye ni Muislam safi.
"Tayari hapo naona kuna shida kubwa. Sisi tulitarajia Tanasha atabadili dini, lakini naona ameanza vikwazo kwa ndugu yetu (Diamond). Tunachojua ni kwamba, Diamond hawezi kuoa mwanamke ambaye hawatakuwa dini moja".
Diamond alitangaza kumuoa Tanasha siku ya wapendanao tarehe 14 February Lakini alihairisha harusi hiyo na Mpaka sasa hawajatangaza tarehe mpya ya harusi.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

DINI NI KIKWAZO KIKUBWA NDOA YA DIAMOND NA TANASHA?
Reviewed by By News Reporter
on
1/31/2019 08:15:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: