Loading...
TAHARUKI imeibuka baada ya mabomu ya machozi kupigwa jirani na mkutano wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, mkoani Njombe.
Masauni aliitisha mkutano huo kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa vijiji kulikotokea mauaji ya watoto 10 mkoani humo.
Wakati mkutano huo ukiendelea kwenye Viwanja vya Turbo mjini Njombe, ghafla jirani na mkutano huo kulisikika milio ya mabomu ya machozi, kitendo ambacho kilisababisha shughuli kusimama.
Baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo, walisogea eneo ambako mabomu hayo yanapigwa kujua chanzo chake na baadaye kudai mbele ya naibu waziri huyo kuwa, kuna mama amekamatwa na mtoto ambaye si wake, ndipo wananchi wakaanza kumkimbiza ili kumkamata.
Masauni alisema maelezo aliyopewa na polisi ni kwamba mabomu hayo yalipigwa ili kutawanya wananchi waliokuwa wakimkimbiza mwizi wa bodaboda.
Kutokana na maelezo hayo ya polisi na wananchi kukinzana, Masauni aliagiza kufanyike uchunguzi na kama ikibainika polisi wamemdanganya, watawajibika.
Katika tukio hilo, Agnes Msigwa, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40-45, alijeruhiwa miguu kwa mabomu hayo na kupelekwa katika Hospitali ya Kibena Njombe ambako Masauni alifika kumjulia hali.
Pia wananchi wawili, mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Gift Sikiga (16), ambaye ni mwanafunzi, waliokolewa na polisi baada ya wananchi kudai wanajihusisha na matukio hayo ya mauaji ya watoto.
Mwanzoni mwa wiki, iliripotiwa kuwa watoto 10 wameuawa mkoani Njombe na kuzua taharuki ambayo ilimlazimu Masauni kukaa na wananchi Wilaya ya Njombe kuzungumzia matukio hayo ya mauaji.
Na Geofrey Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MABOMU YALIVYOVUNJA MKUTANO WA NAIBU WAZIRI
Reviewed by By News Reporter
on
1/30/2019 08:58:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: