Loading...

UN YALAANI VIKALI MAUAJI YA WATOTO TANZANIA

Loading...
Umoja wa Mataifa (UN) umetuma salamu za rambirambi kwa familia na ndugu waliopoteza watoto waliotekwa na kuuawa kikatili Mkoa wa Njombe nchini Tanzania.

Tamko lililotolewa na UN jana Jumanne Januari 29, 2019 limekemea mauaji hayo ikieleza kuwa hayakubaliki na kubainisha kuwa watoto wana haki ya msingi ya kulindwa kutokana na vurugu ili waweze kufurahia na kupata mahitaji yao muhimu.

"Umoja wa mataifa unaungana na Serikali ya Tanzania kupinga vitendo hivyo vibaya. Kama UN tupo tayari kusaidia Serikali katika jitihada zao za kukabiliana na tatizo hilo," anaeleza taarifa hiyo ikimnukuu mratibu mkazi wa UN Tanzania, Alvaro Rodriguez.

"Zaidi ya hayo tunatoa wito kwa wadau wote kuungana pamoja kuhakikisha kunakuwa na usalama wa watoto kuanzia katika makazi, shule na maeneo mengine miongoni mwa jamii."

Watoto wanapitia katika aina nyingi za unyanyasaji katika maeneo mengi duniani, "Hili linatakiwa likome," amesema mwakilishi wa Unicef nchini Tanzania, Maniza Zaman.
Na Vicky Kamata.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
UN YALAANI VIKALI MAUAJI YA WATOTO TANZANIA UN YALAANI VIKALI MAUAJI YA WATOTO TANZANIA Reviewed by By News Reporter on 1/30/2019 08:49:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.