Loading...

LADY JAY DEE ATOA POVU BAADA YA KUCHAMBWA KWA PICHA ZAKE ZA NUSU UCHI

Loading...
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama a Lady Jay Dee amewajia juu watu ambao wamemsema Baada ya picha ya gauni la wazi kusambaa.

Siku ya juzi Lady Jay Dee alizua gumzo kwenye Mitandao ya kijamii Baada ya picha yake iliyomuonyesha akiwa amevaa gauni jeusi lililoacha sehemu kubwa ya maungo yake nje.

Mashabiki walimjia juu Jay Dee kwa kuvaa nguo iliyomuanika maungo yake ya siri huku wengi wakidai wamechukizwa kwa sababu ni msanii na pia ni Kioo cha jamii.

Baada ya Povu hilo Jay Dee ametoa majibu kwa watu hao na kusema wengi wao ni wanafiki kwani hata akivaa mavazi ya heshima huwa hawampongezi pia.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha akiwa sande mjeda, Lady Jay Dee ameandika maneno haya:

"Hivi wale watu wa maadili Mbona picha za Hivi (picha za kistaarubu) huwa hamlike wala hamcomment kwa wingi mkiwekewa?

"Haya maadili hayo hapo sasa inakuwaje? Mbona hamsifii, ila binadamu ni wanafiki sana sijapata kuona".
Na Yohana Makwilo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
LADY JAY DEE ATOA POVU BAADA YA KUCHAMBWA KWA PICHA ZAKE ZA NUSU UCHI LADY JAY DEE ATOA POVU BAADA YA KUCHAMBWA KWA PICHA ZAKE ZA NUSU UCHI Reviewed by By News Reporter on 1/30/2019 08:26:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.