Loading...
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zinazozalisha mchele mzuri na msafi ambao una thamani ukilinganisha unaozalishwa katika nchi za Msumbiji, Kenya, Rwanda na Burundi.
Sambamba na hilo pia imetajwa kuwa nchi yenye idadi kubwa ya wanawake wanaozalisha kwa wingi zao hilo, ambapo huzalisha tani 5-8 kwa hekta, ukilinganisha na nchi ya Msumbiji na Kenya.
Hayo yamebainishwa na mtaalamu wa kilimo kutoka Jimbo la Zambezia nchini Msumbiji, Jaime Gado, alipotembelea nchini akiwa na timu ya wataalamu wa zao la mpunga kwa lengo la kubadilishana ujuzi na kujifunza kutoka kwa wakulima wa Tanzania kuhusu namna ya kuzalisha zao hilo.
Gado mshauri wa mradi ambao unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) alisema mbali na changamoto ya kuwa na mashine zilizochakaa na ubovu wa miundombinu ikiwamo barabara, bado mkulima wa Tanzania amekuwa na hali ya kuzalisha mpunga ulio bora.
Na Gadiel Mussa.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MCHELE WA TANZANIA WAONGOZA KIMATAIFA
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2019 08:29:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: