Loading...
Al Ahly wanatarajia kuikaribisha Simba katika mechi ya raundi ya tatu ya Kundi D itakayochezwa mjini Alexandria, Misri Jumamosi kuanzia saa 4:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ya Rweyemamu imekuja siku chache baada ya baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo kudaiwa kwenda kula "bata" huku wakikabiliwa na mchezo wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa ambao walifungwa na Bandari FC ya Kenya mabao 2-1.
Rweyemamu alisema tayari ameshaanza rasmi kazi katika klabu hiyo na jana alitangulia Cairo kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuipokea timu yao.
Rweyemamu ameteuliwa kurithi mikoba iliyoachwa na Richard Robert ambaye alisimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kile kilichoelezwa kuihujumu Timu ya Taifa "Taifa Stars".
Na Vicky Deus.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SIMBA WAIFUATA AL AHLY KWA HASIRA
Reviewed by By News Reporter
on
1/29/2019 08:39:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: