Loading...
Kenya. Jamaa mmoja kutoka kaunti ya Kisii amefariki dunia baada ya kunyongwa na nyama mbichi siku ya mkesha wa mwaka mpya 2019.
Osoro Oirere kutoka kijiji cha Sameta anasemekana alikuwa anahisi njaa sana na alijikuta aking'ata kipande kikubwa cha nyama ambacho kilikwama kooni.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na mtandao wa TUKO.co.ke, Osoro alikuwa nyumbani kwake wakati kisanga hicho kilipomtendekea.
Chifu wa eneo hilo Linus Choka alisema marehemu alikimbia nyumbani kwa kakake baada ya kugundua kwamba kipande kikubwa cha nyama kilikuwa kimekwama kwenye koo.
Inasemekana mkewe hakuwa nyumbani wala mtu yeyote ambaye angeweza kumsaidia.
Kakake alisema alijaribu kumfanyia huduma ya kwanza ila juhudi zake hazikufaulu.
"Osoro alikuja nyumbani kwangu akikimbia huku akionyesha kidole chake kwenye koo, tulijaribu kumfanyia huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka katika zahanati ya Gentonto ila alifariki muda mfupi kabla ya kuhudumiwa na madaktari," Kakake marehemu alisema.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika kituo cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Lenmek ambapo jamii na marafiki walikusanyika na kuanza kufanya mipango ya mazishi.
Na Catherine Kisese.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

NYAMA MBICHI ILIVYOZUA TAHARUKI, MTU APOTEZA UHAI
Reviewed by By News Reporter
on
1/04/2019 01:54:00 PM
Rating:
Hakuna maoni: