Loading...

SAKATA LA UCHAGUZI DRC: TUME YA UCHAGUZI 'KIZUNGUMKUTI' KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS

Loading...
Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imeahirisha hadi wiki ijayo kutangaza matokeo ya awali ya Uchaguzi wa urais, baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu mwisho wa mwaka 2018.

Raia wa DRC walikuwa wamesubiri kutolewa kwa matokeo hayo, hiyo jana kwa mujibu wa ratiba iliyokuwa imetangazwa hapo awali na Tume ya Uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Corneille Nangaa alisema siku ya Jumapili, isingewezekana kutangaza matokeo hayo kwa sababu mchakato huo bado haujapatikana.

Tume ya Uchaguzi haijatangaza tarehe ya kutolewa kwa matokeo hayo wakati huu, wananchi wakisubiri matokeo hayo kwa hamu licha ya kuwepo kwa hali ya wasiwasi.

Ushindani mkali unashuhudiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wote kutoka upande wa upinzani.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
SAKATA LA UCHAGUZI DRC: TUME YA UCHAGUZI 'KIZUNGUMKUTI' KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS SAKATA LA UCHAGUZI DRC: TUME YA UCHAGUZI 'KIZUNGUMKUTI' KUTANGAZA MATOKEO YA URAIS Reviewed by By News Reporter on 1/07/2019 07:48:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.