Loading...
Mvua kubwa iliyoambatana na upepo na kunyesha kwa zaidi ya saa moja katika Kijiji cha Mgungira, Tarafa ya Sepuka wilayani Ikungi, mkoani Singida, imeezua mapaa ya nyumba kadhaa na kujeruhi watu wanne.
Nyumba zilizoeuliwa ni nne za bati, nyumba nane za tembe na kuwajeruhi vibaya watu wanne.
Desemba 30, mwaka jana mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyodumu kwa dakika 40 iliezua nyumba 56 na kujeruhi watu 9 wilayani Mbozi mkoani Songwe. Pia iliharibu mazao.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mgungira, Diwani wa kata hiyo, Hussein Juma Ng’eni, alisema tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita majira ya alasiri katika Kitongoji cha Mgungira Magharibi baada ya mvua hiyo kunyesha kwa zaidi ya saa moja na kusababisha maafa hayo.
Diwani Ng’eni, hata hivyo aliwataja majeruhi waliotokana na mvua hiyo na ambao wamelazwa katika zahanati ya Kata ya Mgungira kuwa ni pamoja na Kurwa Miete(47), Esher Jeri (15), Rejina Kurwa (5) na Maria Kurwa (5) na kwamba majeruhi hao waliangukiwa na nyumba ya Kurwa Miete
Aidha, diwani huyo alisema kwamba majeruhi wote wanaendelea vizuri na kwamba kwa kuwa mvua zimesimama kidogo jitihada zinafanywa kuhakikisha nyumba zilizobomoka zinakarabatiwa, ili wahusika watakapotoka zahanati waweze kurejea katika makazi yao kama kawaida.
Diwani Ng’eni alitoa wito kwa wananchi wa Kata ya Mgungira na vitongoji vyake kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao itakayosaidia kuzuia kasi ya upepo mkali wakati mvua zinaponyesha.
Na Timoth Zacharia.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MVUA YA SAA MOJA YASABABISHA UHARIBIFU MKUBWA
Reviewed by By News Reporter
on
1/07/2019 07:43:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: