Loading...
Serikali ya Zimbabwe imechukua hatua ya kuwafuta kazi vijana elfu 3 waliokuwa wakifanya kazi katika sekta ya umma kama hatua moja wapo ya kuimarisha uchumi wa nchi hio.
Katika moja ya hatua ambazo zimechukuliwa kwenye uchumi wa Zimbabwe ni kupunguza wafanyakazi katika sekta ya umma. Vijana elfu 3 wafanyakazi wa sekta ya umma wameondolewa kazini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ndani nchini humo, Katibu wa baraza la huduma za jamii Jonathan Wutawunashe, amesema kwamba mishahara katika sekta ya umma imekuwa ni inachukua sehemu kubwa ya bajeti ya nchi hio, na kwa ajili hiyo basi imelazimu kuchukua hatua kwa kuchagua vipaumbele ili kupunguza gharama kwa serikali.
Katika maelezo yake Wutawunashe amesema vijana elfu 3 waliokuwa wakifanya kazi katika wizara mbalimbali nchini humo wameondolewa makazini na kwamba watu hao waliondolewa hawakufuzu vigezo vya kufanya kazi katika sekta ya umma.
Wutawunashe alisema mpango wa kupunguza wafanyakazi ni mpango wa wizara ya Uchumi na maendeleo wa mwaka 2019.Na kwamba katika kurekebisha uchumi hatua zaidi zitaendelea kuchukuliwa aliongeza.
Rais wa Zimbabwe aliyeshinda uchaguzi mwaka uliopita, tangu aingie madarakani amekuwa akipambana kuiondoa nchi hiyo katika mgogoro wa kiuchumi uliodumu kwa miaka mingi.
Na Richard Okechi.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

VIJANA 3000 WAFUTWA KAZI KUUNUSURU UCHUMI WA ZIMBABWE
Reviewed by By News Reporter
on
1/07/2019 08:07:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: