Loading...

'UKUBWA WA MAKALIO HUTUMIKA KAMA KIGEZO KUAJIRI WANAHABARI KENYA'

Loading...
Wakili Maarufu Ahmednasir Abdullahi amefunguka mtazamo wake kuhusu sifa za mabinti wanaotangaza kwenye vituo vya televisheni nchini Kenya.

Wakili huyo Jumapili, Disemba 30 alivikosoa vituo vya habari kutokana na 'vigezo' watumiavyo kuwaajiri watangazaji wanawake.

Wakili huyo alisema siku hizi, watangazaji na wana habari wa vituo vya televisheni huchaguliwa kwa kuzingatia vigezo vya elimu na ukubwa wa makalio yao kwa upande wa wanawake.

"Tuna wataalamu wengi wa kike, kwa mfano Anne Soy, Beatrice Marshall, Sophie Catherine Wambua wanaofanya kazi na vyombo vya habari vya kigeni na kutazamwa kulingana na utaalamu wao wakati wasichana wa humu nchini wanaajiriwa kulingana na urembo wao na 'utajiri' wao wa nyuma," Ahmednasir alisema

Ahmednasir aliibua mjadala huo baada ya kutazama mahojiano yaliyoendeshwa na mwanahabari wa Al Jazeera Catherine Wambua Soi.

Mavazi ya Soi yalikuwa ya kuchochea hisia na kuhakikisha kuwa mahojiano yake yamewavutia wengi. 

Kauli za wakili huyo zimejiri siku chache baada ya baadhi ya Wakenya kukashifu tukio ambapo wanahabari wa kiume pekee walialikwa kumhoji Rais Uhuru Kenyatta kwenye mahojiano ya moja kwa moja ya runinga.
Na Haika Gabriel.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
'UKUBWA WA MAKALIO HUTUMIKA KAMA KIGEZO KUAJIRI WANAHABARI KENYA' 'UKUBWA WA MAKALIO HUTUMIKA KAMA KIGEZO KUAJIRI WANAHABARI KENYA' Reviewed by By News Reporter on 1/01/2019 12:57:00 PM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.