Loading...

WAHUSIKA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE KUKIONA CHA MTEMA KUNI

Loading...
Serikali ya Tanzania imeahidi kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kuhusika katika mauaji ya watoto mkoani Njombe.

Watoto sita, wakiwemo watatu wa familia moja wenye umri chini ya miaka 10 wamepatikana wakiwa wamefariki katika mazingira ya kutatanisha mkoani humo.

Akizungumza Bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema tayari wameshabaini baadhi ya wale waliohusika na mauaji hayo na hatua kali zitachukuliwa.

"Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mauaji hayo yametokana na imani za kishirikina...n tayari tumeshawabaini baadhi ya wale ambao wameshiriki. Nawataka watu waache kuichezea serikali. Tutaanza na mkoa wa Njombe," ameonya Lugola.

Lugola hata hivyo hakusema ni watu wangapi mpaka sasa wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo.
Na Paskali Joseph.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WAHUSIKA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE KUKIONA CHA MTEMA KUNI WAHUSIKA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE KUKIONA CHA MTEMA KUNI Reviewed by By News Reporter on 1/31/2019 09:52:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.