Loading...

WANAOMMENDEA UCHEBE SHILOLE AWAPA MAKAVU

Loading...
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewajia juu na kuwatolea uvivu wanawake wanaomuwinda Mume Wake wa ndoa Uchebe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole amevunja ukimya, awatolea uvivu wanawake wanaomuwinda mume wake akisisitiza ametumia nguvu kubwa kumpa mwonekano alionao sasa.

"Niliridhika na hali yako tangu mwanzo Mpaka sasa unashaini ila wadangaji msivyo na haya mnaanza kumwambia mume Wangu Uchebe amekuwa handsome. Mkome namtunza zamani mlikuwa wapi?".

Shilole alifunga ndoa na Uchebe Desemba ya mwaka 2017 kabla ya hapo Uchebe alikuwa Fundi gereji na asiyejulikana Lakini tangu ameanza mapenzi na Shilole ameonekana kunawiri na Hivi sasa anaishi maisha ya kifahari na msanii huyo.
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WANAOMMENDEA UCHEBE SHILOLE AWAPA MAKAVU WANAOMMENDEA UCHEBE SHILOLE AWAPA MAKAVU Reviewed by By News Reporter on 1/30/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.