Loading...
Shirika la kimataifa la Transparency International limetoa ripoti mpya inayoangazia rushwa katika viwango vya kimataifa. Ripoti hiyo imebainisha hali ya kutisha kuhusu vitendo vya rushwa duniani kwa kusema theluthi moja ya nchi 180 zilipata alama chini ya 50 kati ya 100 wakati alama za wastani kwenye nchi zote zikiwa ni ndogo sana 43.
Kwenye jarida lake kuhusu ufisadi ambalo lilichapishwa tarehe 29 Januari, 2019, Transparency International ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali imesema kushindwa kwa ujumla katika kudhibiti rushwa kunachangia mgogoro wa kidemokrasia duniani kote.
Nchi zilizoonekana kuwa na viwango vya juu vya rushwa ni zile zinazokabiliwa na vita za Somalia, Sudan Kusini na Syria.
Ripoti hiyo pia imetaja kwamba, mara nyingi, taasisi nyingi za kidemokrasia hutishiwa ulimwenguni kote na viongozi wenye tabia za kutumia nguvu au wenye misimamo mikali.
Mkurugenzi wa Transparency International, Patricia Moreira amesema juhudi zaidi zinahitajika ili kuimarisha ukaguzi na uwajibikaji kwa ajili ya kulinda haki za raia.
Aidha, ripoti imetoa wito kwa serikali kuyapa kipaumbele maeneo manne katika kupambana na rushwa:
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

- Kuimarisha taasisi zinazofuatilia nguvu za kisiasa.
- Kuziba pengo la utekelezaji kati ya sheria ya kupambana na rushwa, na utekelezaji wake.
- Kuyasaidia mashirika ya kiraia ambayo yanahamasisha ushirikiano wa kisiasa na ufuatiliaji wa umma juu ya matumizi ya serikali.
- Kuunga mkono uhuru wa vyombo vya habari
Na Neema Joshua.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
RUSHWA CHANZO CHA MGOGORO WA KIDEMOKRASIA DUNIANI
Reviewed by By News Reporter
on
1/30/2019 07:50:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: