Loading...
Msanii wa filamu za Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kusema wazi kuwa taarifa zinazosambaa kuwa amefulia hazina ukweli hata kidogo.
Wema Sepetu amekula shavu baada ya kualikwa kama mgeni rasmi kwenye Usiku wa Zanzibar Sweetheart utakaofanyika Zanzibar Beach Resort hivi karibuni.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti moja hapa nchini, Wema alisema tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni saba hivyo anamshukuru muandaaji wa tamasha hilo kwa kuona umuhimu wake na kwamba ametambua bado anapendwa.
"Bado nina mashabiki wengi sana maana mpaka nimeweza kupata nafasi hii siyo mchezo, ninawashukuru sana waandaaji kunipa nafasi hiyo na hapo kila mmoja ataona muonekano wangu siku hiyo ya tarehe moja mwezi ujao".
Kutokana na ukimya wake kwenye Mitandao ya kijamii imekuwa ikisemekana kuwa staa huyo amefulia na umaarufu wake kuisha baada ya skendo yake iliyomchafua mwaka jana.

Na Christian Komba.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
WEMA AKANUSHA MADAI YA YEYE KUFULIA, ADAI AMELIPWA MKWANJA MREFU WA SHOO
Reviewed by By News Reporter
on
1/28/2019 11:05:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: