Loading...

PAPII KOCHA ATANGAZA KURUDI BENDI YAKE YA ZAMANI

Loading...
Msanii wa muziki wa miondoko ya Dansi nchini, Johnson Nguza Viking 'Papii Kocha' amefunguka na kuweka wazi kuwa ana mpango wa kurudi tena katika bendi yake ya Ngwasuma.

Papii Kocha ametangaza kujiunga na Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' aliyokuwa akiitumikia kabla ya kupatwa na majanga ya kifungo cha maisha na baadaye kupata msamaha wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao mmoja wa habari hapa nchini, Papii Kocha alisema kuwa hafikirii kujiunga na bendi nyingine yoyote zaidi ya kurudi kwenye bendi yake hiyo ya zamani kwani bado anaipenda.

"Kwa sasa nafanya kazi ya muziki kwenye maonesho mbalimbali nikiwa na baba (Babu Seya) kama wasanii binafsi lakini nikishatulia vizuri natarajia kurudi FM Academia na sifikirii kujiunga na bendi nyingine tofauti na hiyo".
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
PAPII KOCHA ATANGAZA KURUDI BENDI YAKE YA ZAMANI PAPII KOCHA ATANGAZA KURUDI BENDI YAKE YA ZAMANI Reviewed by By News Reporter on 1/28/2019 10:18:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.