Loading...
Katika kile kinachoelekea kuwa muujiza baada ya mwanamke mmoja nchini Iraqi, alipofanikiwa kujifungua watoto saba kwa mpigo.
Mwanamke huyo aliyejifungua salama kupitia njia ya kawaida, anasemekana kuwa katika hali nzuri kiafya na watoto wake pia wapo katika hali nzuri.
Kulingana na ripoti ya DailyMail, mwanamke huyo aliyejifungulia katika mkoa wa Diyali ni wa kwanza kujifungua idadi hiyo ya watoto nchini humo.
Msemaji wa hospitali alimojifungulia mama huyo alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa, aliwasili katika hospitali hiyo na kujifungua watoto sita wa kike na mmoja wa kiume.
Baba ya watoto hao Youssed Fadl, alisema yeye na mke wake hawakupanga idadi hiyo ya watoto na sasa wana watoto kumi wa kulea, wakiwamo wa mbeleni watatu.
Pia Fadl alisema mke wake hakuwa na ufahamu angeweza kupata watoto zaidi ya mmoja kabla ya kuupata ujauzito huo.
Na Fatma Pembe.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

BINTI WA MIAKA 25 AJIFUNGUA WATOTO 7 KWA MPIGO
Reviewed by By News Reporter
on
2/20/2019 09:02:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: