Loading...
Wataalamu wamegundua dawa yenye uwezo wa kuondoa hali ya kusahausahau mambo inayowakumba wengi wanapoanza kuzeeka na huenda ikaingia katika maduka karibuni.
Nyakati za 'uzeeni' – kusahau ulikoacha funguo, kusahau sura za watu na kushangaa ni kwa nini uliingia chumbani ni baadhi ya matukio yakukera sana maishani kwa wazee wa miaka zaidi ya 50.
Kwa kuweka umakini sehemu inayomfanya mtu azeeke, utafiti wenye matumaini makubwa umabaini kuwa, huenda karibuni kukawa na dawa ya kurejesha seli katika hali yake ya ujanani.
Inatumainiwa kuwa, kutatolewa tembe ya kila siku baada ya utafiti huo itakayokuwa na nguvu za kufanya akili kuwa ‘changa’. Jarida la Daily Mail la Alhamisi, Februari 15 liliripoti.
Dawa hiyo iliyojaribiwa kwa kutumia panya wazee, imebainika kuwa ina uwezo huo na katika panya hao, tabia yao ilibadilika na kuwa kama ya panya wenye umri wa mtoto mchanga.
Wanasayansi kutoka Kituo cha Uraibu na Afya ya Akili cha Toronto, waliwasilisha utafiti wake Alhamisi, Februari 14, wakati wa Mkutano wa Kila Mwaka wa Shirikisho la Marekani la Uendelezaji wa Sayansi (AAAS) uliofanyika jijini Washington DC.
Dkt Etienne Sibille, aliyeongoza utafiti huo alisema: 'Kwa sasa hamna dawa ya kutibu dalili za kusahau zinazotokea wakati wa msongo wa mawazo, magonjwa mengine ya kiakili na uzee.'
Dawa hiyo mpya ni aina ya ‘benzodiazepiene’ almaarufu kwa lugha ya kisayansi Valium. Lakini tofauti na Valium, yenye athari nyingi, dawa hiyo imetengenezwa kwa malengo maalum ya kuamsha seli za ubongo zilizodumaa zinazohitaji kufanya kazi ya kumbukumbu, Dkt Sibille alisema.
'Utafiti wetu umetambua dawa hii kuwa yenye uwezo wa kutatua hali za kawaida za uzeeni. Itajumlisha kujifunza na kumbukumbu, kupanga, kufanya uamuzi na kupanga.' alisema Dkt Sibille.
Kulingana naye, majaribio salama kwa binadamu yatafanywa katika kipindi cha miaka miwili ijayo na dawa hiyo itakuwa ikimezwa mara moja kwa siku.

Na Frank Richard.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
DAWA YA KUMRUDISHA MZEE KUWA KICHANGA YAGUNDULIWA
Reviewed by By News Reporter
on
2/20/2019 08:47:00 AM
Rating:
Hakuna maoni: