Loading...

JAMAA ALIVYOWAUA WAKE ZAKE 4, KABLA YA KUNYWA SUMU

Loading...
Wakaazi wa kijiji cha Emukaba eneo bunge la Butsotso mashariki kaunti ya Kakamega wamejawa na huzuni baada ya jamaa kumuua mkewe kwa kumdunga kisu usiku wa kuamkia Jumamosi Februari 15, 2019 kufuatia mzozo wa kinyumbani.

William Uningu, mwanamume mwenye umri wa miaka 45 anadaiwa kumuua mkewe mwenye umri wa miaka 37 kabla ya kunywa sumu kwa lengo la kujiua.

Juhudi zake za kujiua hazikufua dafu wenyeji wakijitokeza hima na kumuokoa. 

Kulingana na mdokezi wetu, mshukiwa alimuua mkewe usiku wa kuamkia Jumamosi na akauosha mwili wa marehemu kisha akafululiza kwenda kushuhudia mchezo wa mafahali. 

Aliamua kunywa sumu baada ya kutekeleza kitendo hicho cha kinyama.

"Tumekuwa tukishuhudia mchezo wa mafahali kupigana na jamaa huyu hata tukasalimiana, amekuwa mtu mwenye furaha huwezi kutambua kuwa ametenda kitendo chochote kibaya. Nilipigiwa simu baada ya mchezo kukamilika na nikaambiwa kuwa jamaa niliyekuwa naye amekunywa sumu. Nilipoenda kwake, nilikuta mwili wa mkewe ukiwa umetendewa kitendo hicho cha unyama, amedungwa kisu kichwani na mikononi huku amefungwa kwa wire,'' rafiki yake alisema.

Jamii ilidai kuwa si mara ya kwanza kwa mume huyo kutenda unyama huo na hata kudai kuwa mwanamke huyo huyo alikuwa wanne kutendewa unyama huo.

Aidha afisa anayeshughulikia unyanyasaji wa kijinsia katika ofisi ya gavana Bi Penina Mukabane ameikashifu kitendo hicho na akawasihi wanandoa kusuluhisha tofauti zao kwa amani bila yao kujichukulia sheria mikononi mwao.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha wafu katika hospitali ya rufaa mjini kakamega huku mshukiwa akipokea matibabu katika hospitali hiyo akiwa hali mahututi chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao pia wanaendelea na uchunguzi wa kisa hicho.
Na Baraka Kiringo.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
JAMAA ALIVYOWAUA WAKE ZAKE 4, KABLA YA KUNYWA SUMU JAMAA ALIVYOWAUA WAKE ZAKE 4, KABLA YA KUNYWA SUMU Reviewed by By News Reporter on 2/18/2019 08:12:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.