Loading...
Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.
Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.
Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.
Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar.
Miaka 13 iliyopita mji wa Escobares haukuwepo lakini mwaka 2005 ulitambuliwa kuwa moja ya miji nchini Marekani, kabla ya hapo watu waliyoishi sehemu hiyo hawakua chini ya mamlaka yoyote ya mji.
Baada ya Marekani kusikia kuwa mji wa karibu unaofahamika kama Rome ulikuwa na mpango wa kunyakuwa sehemu ya mji wa Escobares mambo yalibadilika.
98% ya watu wanaoishi Escobares wanatokea taifa jirani Mexico
Baadhi yao walizaliwa mjini humo na wengine wamepewa urai wa Marekani lakini kuna wale ambao hawana "stakabdhi rasmi" waliyotoroka mauaji na utekaji nyara katika jimbo la Tamaulipas.Ukiwa mgeni katika mji wa Escobares ni vigumu kubaini kuwa ni moja ya miji masikini nchini Marekani.
Hakuna visa vya watu kuishi mitaani kama vile vinavyoshuhudiwa mjini Los Angeles, au kukutana na watu wanaoishi katika hali ngumu kutokana na ubaguzi wa rangi katika miji ya Detroit na Baltimore.
Lakini watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Na Paskali Joseph.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.

MJI MASKINI ZAIDI MAREKANI, WATU WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA
Reviewed by By News Reporter
on
2/17/2019 09:19:00 AM
Rating:

Hakuna maoni: