Loading...

KIKWETE ASHTUSHWA NA TAARIFA ZA KIFO CHA GODZILLA

Loading...
Moja ya viongozi waliowahi kuwa karibu sana na wasanii kipindi cha uongozi wake ni rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete , amesema kuwa amepokea kwa mshtuko sana taarifa ya kifo cha mwanamuziki Godzilla kwa sababu alikuwa moja ya vijana wadogo  mwenye ndoto kubwa maishani.

Mhe. Kikwete aliongea maneno hayo huku akiambatanisha na picha yake aliyowahi kuipiga akiwa na msanii huyo miaka ya nyuma.

Aliandika: "Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha msanii wa kizazi kipya GodZila. Alikuwa kijana mdogo mwenye ndoto kubwa na ameondoka wakati ambapo bado mchango wake ulihitajika. Nawapa pole familia ya marehemu na wasanii wote kwa msiba huu. Mwenye Mungu ailaze roho yake mahala pema pema."
Na Catherine Kisese.



Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri mkuu:dundiikaonline@gmail.com.
KIKWETE ASHTUSHWA NA TAARIFA ZA KIFO CHA GODZILLA KIKWETE ASHTUSHWA NA TAARIFA ZA KIFO CHA GODZILLA Reviewed by By News Reporter on 2/15/2019 05:20:00 AM Rating: 5

Hakuna maoni:

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.